12 Septemba 2016 - 20:15
Rais wa Syria aahidi kuendeleza mapambano dhidi ya magaidi

Rais wa Syria Bashar Al Assad amesema ataendelea kupambana na magaidi katika hali yoyote ile huku makubaliano ya kusitisha mapigano yakikabiliwa na changamoto hasa baada ya makubaliano ya awali kuvunjika.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Syria Bashar Al Assad amesema ataendelea kupambana na magaidi katika hali yoyote ile huku makubaliano ya kusitisha mapigano yakikabiliwa na changamoto hasa baada ya makubaliano ya awali kuvunjika.

Huku muda mchache tu ukiwa umebakia kabla ya kuanza kwa mpango wa kusitisha mapigano uliofikiwa na Marekani na Urusi, Bashar Al Assad ameapa kuyarejesha maeneo yote yaliyotekwa na magaidi wanaodhaminiwa na Marekani na kuiweka Syria chini utawala mmoja wenye amani na utulivu kwa raia.

Akisisitiza rais Bashar Al Assad alionekana katika televisheni ya taifa pale alipoutembelea mji wa Daraya ambao kwa muda mrefu ulikuwa umetekwa na magaidi wanaodhaminiwa na Marekani, katika mahojiano pembeni ya barabara Assad alisema ana mkakati wa kurejesha kila eneo la Syria kutoka mikononi mwa magaidi.

Ukimya juu ya kusitisha mapigano

Wakati wote katika mahojiano hayo Bashar Al Assad hakutaja chochote kuhusu makubaliano ya kusitisha mapigano.

Makubaliano hayo yanatarajiwa kuanza muda mfupi ujao kuanzia sasa na yakifanikiwa kuwepo, mpango wa kuwafikishia watu misaada ya kibinadamu unatarajiwa kuimarika na kwa upande mwingine Marekani na Urusi zitaungana pamoja katika zoezi la kupambana na makundi ya kigaidi licha ya Marekani kudhamini baadhi ya makundi ya kigaidi nchini Syria. Juhudi hizi lakini zinakabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo changamoto ya juu ya madai ya Marekani ya kutenganisha baina ya magaidi wa kweli wanaopigania haki na demokrasia nchini Syria na magaidi wanaounga mkono makundi ya kigaidi. magaidi wanaodhaminiwa na Marekani wanadai kuwa mpango huo mzima wa kusitisha mapigano unaipendelea serikali ya Assad ambayo hadi kufikia sasa inaonekana kuwa yenye uwezo zaidi kuliko wao ukilinganisha na wakati mapigano yalipoanza, wanasema nguvu za upande wa serikali zimezidi kutokana na msaada wa kijeshi wa Urusi na Iran.

magaidi hao wanaodhaminiwa na Marekani wanaungwa mkono pia na mataifa zaidi ya 61 ambayo ni washirika wa Marekani katika azima yao ya kutaka kuiangusha serikali ya Syria.

Hatua za kuweka chini silaha

Makubaliano ya hivi sasa ni ya pili yaliyofikiwa na Marekani na Urusi katika mwaka huu ya kwanza yalikuwa mwezi Februari mwaka huu ambayo hayakudumu huku pande zote mbili zikirushiana lawama za kukiuka makubalaiano.

Marekani inaunga mkono baadhi ya makundi ya magaidi lakini sasa inataka kubadili mtazamo wake kuhusianana na swala zima la mapigano nchini Syria hasa katika juhudi za kupambana na kundi linalojiita la kigaidi la Daesh dola la Kiislamu IS ambalo limeyateka maeneo kadhaa nchini Syria na vile vile kundi hilo halimo katika makubaliano ya kusitisha mapigano

Marekani imesema kwamba serikali ya Syria haitofanya mashambulio katika maeneo waliyokubaliana kwa kisingizio cha kuwafuata magaidi na kuwshambulia kutoka katika kundi la Al Nusra Front ingawa magaidi wanaodhaminiwa na Marekani wanadai kuwa kuna uwezekano wa serikali ya Assad kukiuka agizo hilo na hivyo kuendelea kuwashambulia kwa kutumia ndege za kivita.

Kwa mujibu wa habari kutoka kwa naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi, ni kwamba serikali ya Syria na magaidi wanaodhaminiwa na Marekani wa huenda wakakutana mwezi Oktoba katika duru nyingine ya mazungumzo ya amani.

Mwisho wa habari / 291